Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara imeshiriki kwenye Mkutano wa Kikanda Wataalamu wa masuala ya Miliki Bunifu kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC) Johannesburg- Africa ya kusini Novemba 25, 26, 2019.
Lengo la Mkutano huo ni kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa mkakati (Framework) na taratibu za kusimamia na kutumia miliki bunifu katika utekelezaji wa mkakati wa viwanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC.
Tanzania kwa heshima iliyowekwa na Rais Magufuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa SADC imepewa heshima ya kuwa Mwenyekiti pia wa mkutano huo.
Tawi Kilumile Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Leseni za Biashara- (wanne kutoka kushoto) BRELA ndiye Mwenyekiti wa Mkutano huo unaohusisha nchi 15 wanachama wa SADC.
Aidha, katika Mkutano huo Tanzania imewakilishwa na Bakari Mketo Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji wa BRELA.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni -BRELA imewakilisha nchi katika Mkutano huo kwa kuwa ndiyo Ofisi ya Taifa ya Miliki Bunifu (National IP Office).