Nyumba kadhaa katika Kijiji cha Misufini Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro zimezingirwa na maji huku vyakula na mifugo vikisombwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha katika Kijiji hicho na kusababisha mafuriko.
“Mpaka sasa hatutambui wapi tutalala, turuhusiwe tukakae hata shuleni maana hatuna makazi, wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua nyingine, vyakula vimesombwa na maji tangu asubuhi hatujala”-WAHANGA