Serikali imeamua kuifanyia ukarabati mkubwa Shule ya Msingi Mwisenge, ambayo alisoma Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere ili iwe sehemu ya historia ya Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kutembelea shule hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Shule hiyo ambayo ipo Manispaa ya Musoma wanaikarabati ili iwe sehemu ya historia ya Mwalimu Nyerere, pamoja na historia ya Tanzania kwa ujumla.
“Shule hiyo haiwezi kubeba historia ya Mwalimu Nyerere, endapo majengo na miundombinu ya shule hiyo haitakarabatiwa na kujengwa upya, Mipango ya kuifanya shule hiyo iwe sehemu ya historia ya Tanzania inaendelea serikalini na kwamba historia ya Baba wa Taifa itapatikana shuleni hapo.” Waziri Mkuu.