Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, ametangaza kuwaachia wafungwa 5533 ambao walikuwa wamefungwa katika Magereza mbalimbali nchini.
Rais Magufuli akizungumza katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara “Nilitembelea Magereza nikashuhudia kuna mlundikano wa wafungwa, mpaka leo kuna Wafungwa 17,547 na Mahabusu 18,256, hii ni idadi kubwa, kwa hao wafungwa kuna baadhi wamefungwa makosa madogo, sijui kaiba Kuku, kujibizana na mpenzi wake“.
“Hali ya pale Butimba ilinihuzunisha sana, kwa kutambua Dini zote zinatufundisha tusamehe na kuamini wafungwa wengi wanajutia makosa yao, kwa mujibu wa Mamlaka niliyonayo ya Kikatiba, nimewasamehe wafungwa 5533“ Rais Magufuli