Gavana wa Jimbo la Nairobi Mike Mbuvi Sonko hatimaye ameachiliwa kwa dhamana ya ya zaidi ya Milioni 330 lakini amekatazwa kufika katika ofisi yake.
Katika uamuzi uliotolewa katika Mahakama ya Milimani siku ya Jumtano, pia amezuiwa kufika katika ofisi yake isipokuwa iwapo atakuwa na Afisa wa Uchunguzi ama mtu yeyote aliyeruhusiwa na Mahakama.
Atakapoenda katika ofisi yake akiandamana na afisa aliyeruhusiwa, ataruhusiwa kubeba vitu vyake pekee.
Sonko na washukiwa wenzake pia wamepigwa marufuku kutosafiri na watahitaji ruhusa ya mahakama kabla ya kufanya hivyo.
Mkuu huyo wa Jimbo la Nairobi pia ametakiwa kuhakikisha kwamba wafuasi wake wanaweka amani katika Jimbo hilo.
#ViaCitizen
PART 2: “NIMEACHWA NA WANAUME WAWILI CHRISTMAS, MMOJA AMEOA”