Leo December 11, 2019 Mkurugenzi wa TBS Mkurugenzi TBS Dkt. Athuman Ngenya ameelezea mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka minne ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli madarakani.
“Viwango hivyo vimesaidia wafanyabiashara, wajasiriamali, wenye viwanda na wadau mbalimbali kuzalisha bidhaa bora zinazoleta ushindani” Dkt. Athuman Ngenya, Mkurugenzi TBS
“Shirika limefanikiwa kutayarisha jumla ya viwango 1,587 katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya chakula, kemikali, mazingira, sekta mtambuka, ngozi na nguo, uhandisi (umeme, mitambo, ujenzi na madini)” Dkt. Athuman Ngenya
“TBS ina jukumu la kudhibiti ubora wa bidhaa, hivyo bidhaa zinazozalishwa nchini na zinazoingia nchini huhakikiwa ubora kwa kupimwa katika maabara zetu. Jumla ya sampuli 71,863 zilipimwa katika maabara za TBS sawa na 85.6 % ya lengo la kupima sampuli 84,000” Dk. Athuman Ngenya
“Vilevile katika kipindi cha miaka minne jumla ya mitambo na mashine 21,726 zilifanyiwa ugezi ambapo ni sawa na 82.5% ya lengo la kufanyia ugezi mashine 34,000” Dkt. Athuman Ngenya, Mkurugenzi Mkuu Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
“TBS ina maabara 8, kati ya hizo maabara 6 zimehakikiwa na kupatiwa vyeti vya umahiri(Accreditation). Ripoti zinazotolewa na maabara hizo zinatambulika na kukubalika kimataifa na hivyo kumuwezesha mfanyabiashara kupata urahisi wa masoko ya kimataifa” Dk. Athuman Ngenya
“Maabara zifuatazo zimehakikiwa na kupatiwa vyeti vya umahiri (Accreditation): a) Maabara ya Ugezi, b) Maabara ya Chakula, c) Maabara ya Kemia (mafuta ya petroli), d) Maabara ya uhandisi Umeme; e) Maabara ya uhandisi mitambo; na f) Maabara ya ujenzi” Dkt. Athuman Ngenya
“Shirika limefanikiwa kumaliza ujenzi wa jengo jipya la maabara ya kisasa lea ghorofa 8 litakalorahisisha utendaji wa shughuli za maabara na kutatua changamoto iliyokuwepo awali ya ucheleweshwaji wa majibu ya sampuli na ufinyu wa eneo”Dk. Athuman Ngenya-Mkurugenzi Mkuu wa TBS
“TBS imeendelea kutekeleza Sheria ya Bajeti kwa kuwasilisha Serikalini 15% ya mapato ghafi na kuchangia mfuko wa serikali. Kuanzia mwaka 2016/2017 mpaka septemba, 2019 TBS limewasilisha serikalini jumla ya Sh. bilioni 34.8″ Dkt. Athuman Ngenya, Mkurugenzi Mkuu wa TBS
“TBS imeendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo, wafanyabiashara, wenye viwanda na umma kwa ujumla kuhusu viwango na udhibiti ubora wa bidhaa. Kwa kipindi cha miaka minne tumefanikiwa kutoa jumla ya semina za mafunzo 206″ Dk. Athuman Ngenya, Mkurugenzi Mkuu TBS
“TBS imefanikiwa kufungua ofisi katika kanda na mipaka ikiwa ni moja ya hatua ya kusogeza huduma karibu na wananchi ili kupunguza ucheleweshaji wa utoaji wa huduma hizo pamoja na kuwapunguzia wazalishaji gharama ya kufuata huduma za Shirika Dar es Salaam” Dkt. Athuman Ngenya
PART 2: “NIMEACHWA NA WANAUME WAWILI CHRISTMAS, MMOJA AMEOA”