Siku moja tangu kuripotiwa kwa Watu 45 kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kufuatia kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu wakiwa Msibani, Wizara ya Afya imesema idadi ya Watu imeongezeka.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Faustine Ndugulile amesema hadi sasa wamefikia Wagonjwa 53 na bado uchunguzi unaendelea kufanyika kujua kiini cha tatizo.