Polisi Mkoani Iringa wanaendelea kumshikilia Mwalimu Arnord Mlay (30) kwa tuhuma za kuwalawiti Watoto watano wenye umri wa miaka 10 – 16, ili kuwapa nafasi Wazazi ambao Watoto wao wamefanyiwa ukatili huo kuendelea kutoa taarifa Polisi, inadaiwa zaidi ya Watoto 20 wamekumbwa na kadhia hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa amesema kati ya Watoto anaotuhumiwa kuwalawiti wanne ni wa Shule ya Msingi ma mmoja Sekondari na inadaiwa alikuwa akiwafundisha Tuition nyumbani kwake.
“Tangu 2016 Mtoto mmoja alianza kulawitiwa na kutishiwa kuuawa kama angetoa siri, juzi hapa akawaandikia barua wazazi wake kwamba hataki tena Tuition wakimlazimisha atajiua, alipoulizwa chanzo akasimulia na kuwataja Watoto wenzake wanaofanyiwa hivyo”-RPC Iringa
“Wazazi wanatumia muda mwingi na majukumu yao wakiwa nyumbani wanakuwa bize na mitandao pasipokuangalia Familia na kuwaachia Wasaidizi wa kazi pekee, pangeni muda kuongea na Watoto wenu kujua changamoto zao” – RPC Iringa
TAZAMA VIDEO KUKU ALIYEUA MTOTO WA MIEZI SITA ALIVYOUAWA , MAMA AZUNGUMZA