William Moye Mkazi wa Moshi Mkoani Kilimanjaro amechukua headlines baada ya kuwafanyia suprise waliohudhuria kwenye Harusi yake kwa kuingia ukumbini akiwa ndani ya Helicopter na Mkewe, wengi walishangaa na kupiga shangwe kwa furaha kwakuwa hawakutarajia kitu hicho kutokea.
Moye na Mke wake wamezungumza na AyoTV na millardayo.com na kusema Harusi ni kitu cha mara moja hivyo Watu wakipata fursa wasihofie kutumia pesa ili iwe ya nguvu, wanaamini watadumu kwenye ndoa yao licha ya Imani zilizojengeka vichwani mwa baadhi ya Watu kuwa waliotumia gharama kubwa huwa hawadumu.