Polisi Wilayani Igunga, Tabora wamemfikisha Mahakama ya Wilaya hiyo Mfamasia Francis Mlesa (33), anayefanya kazi Hospitali ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma za kuiba chupa 30 za ARVs .
Mshtakiwa amekana kutenda kosa na kesi imeahirishwa hadi January 31, 2020, Mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana.
Mfamasia huyo alikamatwa na mlinzi akiwa na Box zenye dawa hizo ambazo inadaiwa anawauzia wafugaji ili kunenepesha mifugo.