Upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha wa zaidi ya Sh.Mil 10 inayowakabili Afisa Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti (26) na mwenzake mtaalamu wa masuala ya Tehama, Theodory Gyan (36), upo katika hatua nzuri.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Renatus Mkude mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa, hivyo wameomba shauri liahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada kueleza hayo, upande wa utetezi wenye Mawakili saba, ukiwakilishwa na Fulgency Massawe umedai kuwa wanaomba uanze upelelezi kabla ya Mtu kukamatwa.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 21, 2020 na washitakiwa wamerudishwa Mahabusu kwasababu kesi yao haina dhamana.
MWANRI AWAVAA WANAOBEZA MAAGIZO YAKE “UNATAKA NIWAPIGE NGUMI”