Polisi Mkoani Mwanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya kiusalama wamewakamata Watu saba wanaojifanya Maofisa Usalama wa Taifa kutoka Ikulu ya Tanzania, wanatuhumiwa kuwatapeli Wananchi na Watumishi Serikalini huku wakiwajengea hofu ili kutengeneza mazingira ya kupewa rushwa.
“Watuhumiwa walikuwa wakitumia Toyota la kubeba wagonjwa lenye usajili No. T.751 BNL ambalo huwa wanaunga nalo nyuma ya Misafara ya Viongozi Wakuu wakijifanya ni sehemu ya Misafara, tumewakuta na vitambulisho vya Ikulu, pia wana vitambulisho vinavyoonesha ni Marubani wa Ndege ya Rais”-Jumanne Murilo, RPC Mwanza
“Watuhumiwa Walikamatwa na Makachero na bado wakaendelea kujitambulisha kuwa wao ni Maofisa Usalama wa Taifa kutoka Ikulu lakini walipohojiwa kwa kina ilibainika ni Matapeli”- RPC MWANZA