Rais wa Marekani Donald Trump amesema hakuna Mwanajeshi wa Marekani aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na Iran kwenye Kambi za Jeshi la Marekani nchini Iraq.
Mapema leo Televisheni ya Taifa ya Iran imetangaza kuwa Wanajeshi 80 wa Marekani wameuwawa katika shambulio hilo la Makombora.
“Katika miaka mitatu ya Utawala wangu, America imekuwa imara zaidi. Kwa sasa tunajitegemea na hatuhitaji tena msaada wa Mashariki ya Kati kwa sababu tunaongoza kwa uzalishaji wa mafuta ghafi na gesi asilia” Trump
“Soleiman alikuwa Kiungo muhimu sana katika kushamiri kwa ugaidi katika Mashariki ya Kati na Duniani kwa ujumla. Kitendo cha sisi kumuondoa kimetuma Ujumbe mzito kwa Magaidi, kwamba kama unathamini maisha yako, hautahatarisha maisha ya Watu wetu” Trump
“Wakati tukiendelea kutathimini hatua dhidi ya uchokozi wa Iran, Marekani inakwenda kuuadhibu Utawala wa Iran kwa Vikwazo vya Kiuchumi. Vikwazo hivi vikali vitaendelea hadi hapo Iran itakapobadilisha tabia yake” Trump
CHANZO CHA UADUI MKUBWA IRAN NA MAREKANI, VITA ILIYOUA WATU MAMILIONI, NDEGE KUDUNGULIWA