Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo walicheza mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup 2020 dhidi ya Bingwa mtetezi Azam FC katika uwanja wa Amaan, Simba SC ambao walikuwa na kumbukumbu mbaya dhidi ya Azam katika michuano hiyo baada ya mwaka jana kupoteza dhidi ya Azam FC hatua ya fainali.
Safari hii imeonekana wamekuja kitofauti na kuwa makini zaidi licha ya timu yao kukosa nafasi kadhaa za wazi wakati wa mchezo, dakika 90 ziliisha bila timu yoyote kupata matokeo chanya (0-0), ndipo muamuzi alipoamua kuitisha mikwaju ya penati kama sheria za mashindano hayo zinavyosema na kumalizika kwa Simba SC kushinda kwa penati 4-2.
Matokeo hayo ni wazi Simba SC katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo atacheza January 13 2020 dhidi ya Mtibwa Sugar ambao jana, walifuzu kucheza fainali kwa kumfunga Yanga SC kwa penati 4-2, hiyo ni baada ya mchezo huo dakika 90 kuisha 1-1.
VIDEO: DIDA ALIACHWA SIMBA KISA KAOMBA MKATABA AKAUOSOME KABLA YA KUSAINI