Sultan Qaboos bin Said Al Said wa Oman, mtawala wa muda mrefu zaidi katika Falme za Kiarabu, amefariki akiwa na umri wa miaka 79. “Kwa huzuni kubwa, Oman inaomboleza kifo cha Mfalme wake Sultan Qaboos bin Said, ambaye alifariki Ijumaa (jana),” Ilisema taarifa iliyotolewa na serikali ya Oman.
Mwezi uliopita (Disemba) alirudi nyumbani baada ya kupata matibabu nchini Ubelgiji. Kulikuwa na taarifa kuwa alikuwa akiugua saratani. Zimetangazwa siku tatu za maombolezo ya Kitaifa.
Hadi anafariki hapo siku ya Ijumaa (jana) Sultan Qaboos hakuwa ameoa tena baada ya kufunga ndoa mwaka 1976 na binamu yake, ilidumu miaka mitatu tu (hakubahatika kupata mtoto) na hakuwa na mrithi au mteule aliyemteua.
Kulingana na Kauli ya Msingi ya Usultani, Baraza la Familia la Kifalme – ambalo linajumuisha washiriki wanaume 50, linapaswa kuchagua Sultani mpya ndani ya siku tatu za kiti cha enzi kilichoanguka.