Askari wa Kitengo cha Upelelezi Jijini Arusha, Sajenti Michael Njau mwenye nambari E2548 amekamatwa na Maofisa wa TAKUKURU akipokea rushwa ya kiasi cha Tsh. 650,000
Njau alikamatwa akipokea rushwa katika eneo la Father Babu mkabala na eneo la kuuzia magari kufuatia mtego uliowekwa na Maofisa wa Idara hiyo
Ofisa huyo alikamatwa mara baada ya mtego uliowekwa na TAKUKURU baada ya Njau kutaka rushwa kutoka kwa mkazi mojawapo wa Arusha aliyekuwa na shida ya kusaidiwa ndugu yake ambaye amekamatwa na kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi
Kwa sasa anashikiliwa na TAKUKURU huku taratibu nyingine za kumfikisha mahakamani zikiendelea
MAGUFULI “KILA KITU KIKIFANYIKA NI USALAMA WA TAIFA, MTU HAJAPOTEA WANASINGIZIA WASHUGHULIKIWE”