Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesikitishwa na uamuzi wa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini wa kujiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Upinzani Bungeni na kusema wazi sababu alizotoa hazina mashiko.
Mbowe ameshangazwa na taarifa ya Selasini kwamba hakuwahi kupewa Barua ya Uteuzi. Ameuliza, kama hakupewa barua ya uteuzi imekuwaje aandike barua ya kujiuzulu?.
Mbowe amesema, Selasini amekuwa Mnadhimu kwa miaka miwili, anaheshimiwa na Wabunge wote wa Upinzani huku akipewa ushirikiano wote na Ofisi ya Bunge, amekuwa akihudhuria Vikao vyote vya Kamati za Uongozi na kulipwa posho.
Kiongozi huyo Mkuu wa Upinzani Nchini ameonyesha wazi kutofurahishwa na uamuzi huo wa Mbunge Selasini na kusema labda kama ana mambo yake ya Siri ndiyo maana ameamua kufanya hivyo.
“MTU WA ARUSHA KUWA M-BONGO NI BONGE LA DHAMBI” MACHALII WA CHUGGA WAMEKUJA KUFANYA MAKUBWA DAR