Maseneta 100 wa Marekani wameapishwa jana kama Baraza la Mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili Rais Donald Trump ya Matumizi Mabaya ya Madaraka.
Katika kesi hiyo itakayosikilizwa Januari 21, Maseneta hao wataamua iwapo Rais Trump anastahili kuondolewa madarakani kwa makosa yaliyowasilishwa na Bunge la Wawakilishi.
Trump anashtumiwa kwa kutumia vibaya madaraka na kuingilia Bunge ambapo yeye mwenyewe amekanusha kutekeleza makosa hayo na kusema kwamba kesi dhidi yake ni madai dhidi yake ni ya uongo.