Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewapa wiki moja wawekezaji wa kiwanda cha karatasi cha Mufundi kufika ofisini kwake Mkoani Dodoma.
Akizungumza katika ziara yake katika kiwanda hicho kilichopo mkoani Iringa, Bashungwa ameshangzwa na jinsi wawekezaji hao walivyoshindwa kukiendeleza kiwanda hicho.
Bashungwa amesema kiwanda hakionyeshi kama kinakwenda na dhumuni la kuanzishwa kwake hapa nchini.
“Mwalimu Nyerere na Rais John Pombe Magufuli sera zao ni sawa za kuendeleza viwanda nchini, lakini hapa sioni kama jambo hilo litafikiwa, kiwanda hiki kilijengwa kwa gharama ya Dola 260 Milioni na kilipobinafsishwa kiliuzwa Dola 26 Milioni kwa wawekezaji ikiwa ni pungufu ya asilimia 90 ya thamani yake ya awali” Bashungwa
Bashungwa alisema fedha hizo dola 26milioni hazikuingia Serikalini alipewa mwekezaji wa lengo la kufanyia ukarabati kiwanda ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi “Hadi sasa sijui kama hata kodi mnalipa kwa serikali, natoa wiki moja nataka uje Dodoma kwa ajili ya kulizungumza suala hilo”
Bashungwa aliongeza sera ya kiwanda hiki kilitengezwa kwa ajili ya kuondoa tatizo la upatikanaji wa karatasi nchini.
Bashungwa alisema masuala ya Usalama ya Taifa yana mambo mengi hata hili linaweza kuwa iwapo mataifa mengine yakikataa tuuzia karatasi itakuwa ni tatizo kubwa “Watu watatushangaa tunashindwa kutengeza hata karatasi kwa ajili ya watoto wetu waliopo shuleni”
BREAKING: TCRA WATANGAZA HABARI MPYA “HATUTAZIMA LAINI ZOTE AMBAZO HAZIJASAJILI LEO