Mbunge wa Morogoro Mjini Azizi Abood amefanya kikao na Wajasiriamali wadogo pamoja na bodaboda “Leo ni siku muhimu sana kwenu Wajasiriamali na waendesha Bodaboda, naomba muitumie kueleza masuala mbalimbali ambayo ni kero kwenu mbele ya Viongozi wa Taasisi mbalimbali hapa ili panapohitaji elimu mpewe, panapohitaji hitaji ufafanuzi mfafanuliwe na panapohitaji kuchukua hatua basi Taasisi hizi zenye dhamana wakachukue hatua”.
“Rais Magufuli na Serikali ya awamu ya tano inawapenda sana Wajasiriamali na ndio maana kila siku wanaendelea kutengeza mazingira bora ili muendelee kufanya shughuli zenu kwa amani na utulivu” Aziz Abood
“Nawasihi ndugu zangu wajasiriamali na waendesha bodaboda ni wakati muafaka muunde chama chenu madhubuti kitakachowafanya muwe wamoja na mkawa na Viongozi wenu wanaofahamika ili tuweze kushirikiana na kushirikishwa katika masuala mengi yanayohusu kundi lenu” Aziz Abood
“Napenda tuendelee kushirikiana kwa karibu Sana, nawapenda sana na ndio maana nilionana na baadhi yenu na kuona malalamiko yenu yanafanana nimeona niitishe mkutano huu ili tuweze kuweka mambo sawa” Aziz Abood
“Naamini baada ya kikao hiki muhimu, nimeona wataalamu na maafisa mbalimbali wameeleza masuala mengi sana ikiwemo kueleza matakwa ya sheria mbalimbali, baada ya hapa kila moja ataendelea na shughuli zake katika misingi ya Sheria na taratibu.”Aziz Abood