Nje ya mpira wa kikapu Bryant alikuwa moja ya watu maarufu wanaohamasisha jamii kufuatia mafanikio makubwa aliyoyapata kwa kucheza mpira wa kikapu, hakuwa mchoyo amekuwa akitoa mbinu mbalimbali za namna ya kupata mafanikio, ambapo wengine walimfahamu zaidi kufuatia jumbe hizo za kuhamasisha alizokuwa akiweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Bryant ni mzungumzaji mzuri ambaye amekuwa akitoa hamasa mbalimbali kuhusu namna ambavyo amefanikiwa na amekuwa akitoa maneno yanayoishi na kugusa watu wengi.
Wengi tutaishi maneno yake ambayo yalikuwa ni ya kujenga zaidi, hizi hapa sentensi tano alizowahi kuzitoa Bryant.
1.Changamoto ni fursa kwangu kuinuka na kufanya jambo.
2. Wazazi ni uti wa mgongo wangu, ndio kundi pekee litakalokuwa pamoja nami katika nyakati zote, nikiwa chini au nikiwa juu.
3. Sitaki kuwa Michael Jordan anayefuata, Nachotaka ni kuwa Kobe Bryant.
4. Muda unakata tamaa, ndio muda mtu mwingine anafanikiwa
5. Mambo makubwa huja kufuatia juhudi katika kazi, sio kwa kuleta sababu zitakazokufanya usijafanye jambo Fulani.
Bryant alizaliwa Agosti 23, 1978 na kufariki dunia siku ya Jumapili ya Tarehe 26 Januari 2020 na mtoto wake Gianna katika helikopta yake binafsi iliyopoteza uelekeo na kugonga mlima kisha kulipuka na kupelekea vifo vya watu tisa waliokuwepo kwenye helikopta hiyo.
Bryant ameacha mke, Vanessa Laine Bryant na watoto watatu Natalia Diamante Bryant, Bianka Bella Bryant, Capri bryant ambapo mtoto mmoja aliyefuata nyayo zake za kucheza mpira wa kikapu ametangulia naye mbele za haki, Gianna.
BREAKING: Magufuli amtumbua Lugola “unanitesa, ondoka hapa sina urafiki kazini” (+video)