Shirika la Afya la Ulimwenguni (WHO) linatarajia kuitisha Kikao cha Kamati yake ya Wataalamu hii leo ili kujadiliana iwapo wanaweza kutangaza mlipuko wa Virusi vya Corona kama Dharura ya Afya Duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Gebreyesus amesema, ni muhimu kuitisha mkutano mwingine ambao ni wa 3 kwa wiki hii kwa kuwa Virusi hivyo vimekwishasambaa hadi nje ya China, hali inayozidi kutia wasiwasi.
China imesema, idadi ya Visa vipya vya maambukizi imepanda na kufikia 571 na kufanya jumla ya visa hivyo kufikia 7,700 na watu 170 wamekwishafariki hadi kufikia mapema leo.