Chama cha soka cha Zambia (FAZ) sasa imemtangaza rasmi Milutin Sredojevic “Micho” kuwa kocha wao mkuu mpya wa timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo.
Micho ,50, ametambulishwa rasmi na Zambia kama kocha wao mkuu mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ambapo atakuwa na mtihani wa kuipambania timu hiyo ifuzu AFCON 2021.
Kocha huyo raia wa Serbia ametambulishwa leo na Rais wa FAZ Andrew Kamanga, sasa Micho anaelekeza nguvu zake katika mchezo wa March 26 2020 wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Botswana.