Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda leo February 05 amethibitisha kupokea kiasi cha Shilingi Milioni 600 zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa majengo matano ya kisasa ya Kituo cha Afya Bunju A kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi.
RC Makonda amesema wakazi wa Bunju na maeneo ya jirani waliohitajika kufanyiwa Upasuaji walikuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu hadi Hospital ya Mwananyamala kwa ajili ya huduma hiyo na kutokana na umbali mrefu baadhi yao hufariki Dunia wakiwa njiani na wengine kutumia gharama kubwa ya usafiri.