February 6, 2020 Watu watatu wamefariki dunia baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuteleza na kuharibika vibaya wakati ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gokcen.
Ndege hiyo kutoka Shirika la Pegasus yenye namba PC2193 ilikuwa na jumla ya abiria 183, iliteleza kwa umbali wa Mita 60 na kuwaka moto. Ndege hiyo iligawanyika katika vipande viwili.
Waziri wa Afya, Fahrettin Koca amesema mbali na vifo hivyo, majeruhi takriban 179 wamepelekwa katika Hospitali tofauti.
Ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni hali mbaya ya hewa.
HISTORIA: DANIEL ARAP MOI JABARI LA SIASA AFRIKA, JASUSI ALIEPINDULIWA, UFISADI