TFF imetangaza kumfungia kwa miaka 3 muamuzi msaidizi Kassim Safisha kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea (Offside) wakati wa mchezo namba 150 wa Simba VS Namungo FC, uliyomalizika kwa Simba kupata ushindi wa 3-2.
“Mechi namba 150: Simba SC 3 v Namungo FC 2-Mwamuzi msaidizi namba mbili Kassim Safisha amefungiwa miaka mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea katika mechi hiyo Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 39(1)(a) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi”
Kassim ameingia katika matatizo baada ya kuruhusu goli la Kagere dakika ya 89 ambalo likaifanya Simba kuondoka na ushindi na kuvuta point 3 ila picha za marejeo ya video zikaonesha kuwa Kagere alikuwa Offside.