Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura (OCHA), Bwana Mark Lowcock amesema wimbi la nzige waliozingira ukubwa wa Kilometa moja za mraba, huwa na nzige Milioni 40 – Milioni 80, ambao wanaweza kula kwa siku moja chakula ambacho kinatosheleza kulisha watu 35,000
–
Akitolea mfano uvamizi wa nzige hao Kaskazini Mashariki mwa Kenya amesema wimbi la nzige lilikadiriwa kuwa ni la ukubwa wa Kilometa za mraba 2,400 na nzige hao wanaweza kula chakula ambacho kinaweza kulisha watu milioni 84 kwa siku.
Wimbi la nzige limevamia sehemu ya Afrika ambayo tayari ina changamoto nyingine kama ukame, njaa, mafuriko na machafuko yanayoendelea. Watu milioni 30 hawana uhakika wa chakula kwenye maeneo ambayo yamekumbwa na majanga hayo.
Nzinge ni wadudu wa kale sana ambao uhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na uvamizi wao unaweza kusambaratisha kabisa mazao na malisho haraka sana.
AGE IS JUST NUMBER, MWANAUME AOA MWANAMKE ALIEMZIDI ZAIDI YA MIAKA KUMI