Hatima ya kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili, Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera itajulikana Februari 17, 2020 baada ya Upande wa Mashtaka kuomba kuzungumza na mwandishi huyo kwa siri kwa ajili ya kuingia naye makubaliano.
Hatua hiyo inakuwa ni ikiwa ni wiki chache baada ya Kabendera kuomba kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP) kwa ajili ya maelewano.
Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega kuwa kwa muda mrefu kulikuwa na mchakato wa maelewano baina ya Mshitakiwa na Mkurugenzi wa Mashitaka, hivyo wapo katika hatua ya mwisho.
Amedai kuwa hatua iliyobakiwa ni kuzungumza na mshitakiwa mwenyewe baada ya kuzungumza na mawakili wake, hivyo wanaomba kesi hiyo iahirishwe hadi Jumatatu, Februari 17, 2020.
“Tunawasilisha maombi ya kuzungumza na mshitakiwa kwa sababu tayari tulishazungumza na mawakili wake,”amesema.
Hakimu Mtega amesema kuwa kutokana na ombi hilo la upande wa mashitaka anawakubalia, hivyo anaahirisha kesi hiyo hadi Februari 17, 2020.
KILICHOSEMWA MAHAKAMANI KESI YA ERICK KABENDERA “TUNAOMBA KESHO”