Askari wa JWTZ Wilayani Nachingwea, Lindi Pascal Lipita(28), amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi Askari mwenzake ambaye ni Mpenzi wake Baserisa Ulaya, chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa huo Maria Butulaine, Pascal anadaiwa kummiminia risasi 19 Mpenzi wake huyo na kumsababishia kifo wakiwa kwenye kambi ya Nang’ondo,Nachingwea.
Mshtakiwa amerejeshwa rumande na atarudi tena Makamani March 02, 2020 kesi itakapotajwa.