Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa Hukumu ya kesi inayowakabili Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Jamii Forum Maxence Melo na mwenzake Micke William kutokana na Hakimu anayeendesha shauri hilo kutohudhuria mahakamani hapo.
Hii leo kesi hiyo ilitarajiwa kutolewa hukumu ambapo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambaye anasikiliza shauri hilo amepangiwa majukumu mengine.
Kutokana na hatua hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 2, 2020 kwa ajili ya hukumu.
Melo na mwenzie wapo nje kwa dhamana na kwa mujibu wa kisheria kesi inayomkabili mshitakiwa huyo haruhusiwi kutoka nje ya mipaka bila ruhusa maalumu ya mahakama.
DAWA YAMBADILISHA KUWA ALBINO “ANAPANDISHA MAJINI, NGOZI KAMA NYOKA INAPUKUTIKA”