Leo February 21, 2020 Tangu mwisho wa wiki iliyopita bei ya gesi inayotumika kwa matumizi ya nyumbani imepanda kwa zaidi ya wastani wa Tsh. 5,000 kulinganisha na ilivyokuwa awali.
Kwa mitungi midogo, Wananchi wanasema gesi aina ya Oryx ndio imepanda zaidi kutoka Tsh. 19,000 hadi Tsh. 22,000 huku gesi aina ya Mihan ikitoka Tsh. 16,000 hadi 17,500.
Aidha, katika ujazo mwingine wa gesi, Mtungi wa Kilogram 15 umepanda kutoka Tsh. 48,000 hadi Tsh. 54,000 huku mtungi wa Kilogram 35 ukipanda bei kutoka Tsh. 75,000 hadi Tsh. 105,000.
Watumiaji wamesema kupanda kwa gesi hiyo inayotumika kwa wingi majumbani unaongeza ugumu wa maisha kwa kuwa bei ya vitu vingine vimepanda pia.
Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo amesema upandaji huo wa gesi ya nyumbani unasababishwa na soko la dunia.
MWANRI ALIAMSHA “WANYANG’ANYWE KIWANDA, KIBARUA KITAOTA UKOKO, NILIENDA NA BASHE USIKU”