Waziri Mkuu Kasim Majaliwa leo ametembelea banda la maonesho la STAMICO na kupongeza shughuli za Shirika katika uwekezaji, Maonesho hayo ya siku mbili yanayofanyika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere DSM yamendaliwa na Wizara ya Madini na yanaenda sambamba na Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini.
Akizungumza wakati anatembelea banda la STAMICO, Majaliwa ameipongeza STAMICO katika uwekezaji wake katika Sekta ya Madini kupitia miradi yake mbalimbali.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dk.Venance Mwasse amesema Shirika linaendelea vizuri na shughuli zake za uwekezaji pamoja na changamoto inazopitia “Shirika limejipanga kuendeleza miradi yake ikiwa ni pamoja na kuongeza mashine za chorongaji ili kukidhi mahitaji ya wateja ”
Mwasse amesema kwa sasa mgodi wa STAMIGOLD unaendeshwa kwa faida na umepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uzalishaji “Mgodi wa STAMIGOLD unamilikiwa na STAMICO na unaendeshwa na wazawa kwa 100%”
Katika Mkutano huo Majaliwa pia amezindua hati ya uhalisia ya Madini ya bati ambayo itaiwezesha Tanzania kuuza Madini ya Bati popote Duniani.