Sekta ya ujenzi Tanzania inakadiriwa kukua ikiwa ni sehemu ya matokeo ya juhudi za Rais Magufuli za kukuza viwanda nchini, ongezeko la mahitaji ujenzi salama usiochukua muda na gharama ni mojawapo ya mahitaji muhimu kwa sasa katika sekta hii.
Ujenzi wa SAFBUILD usiokuwa na gharama ambao unatumia nguzo za vyuma katika pande zote za jengo, umeleta mapinduzi katika sekta ya ujenzi kwa kukidhi mahitaji ya ubunifu, gharama nafuu na wepesi katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwakilishi wa Alaf Limited, Mhandisi. Erick Sumary alisema kwa kutarajia ukuaji mkubwa katika soko hili jipya la ujenzi, tunawaletea SAFBUILD, ili kukidhi mahitaji ya wateja wanaohitaji huduma hii nafuu, lakini pia ni rafiki katika utunzaji wa mazingira. Tumefanya uwekezaji kwenye SAFBUILD kwa kuboresho ya vyuma vya kawaida badala ya kuziondoa kabisa.
SAFBUILD inalenga wawekezaji wenye lengo la ujenzi kutumia vyuma katika hatua ya awali, kama vile viwanda, ghala, vituo vya kuhifadhia, na mimea ya viwandani. Ili kupunguza gharama za uendeshaji, SAFBUILD imebuniwa katika muundo wa kisasa wa SAFDESIGN ambao unatoa fursa kwa muhusika kufikia malengo yake kwa muda mfupi kuanzia kwenye wazo hadi kufikia mradi wenyewe, kwa kuzingatia mfumo wa kimataifa katika mazingira ya kawaida alisema Sumary.
Ripoti ya Utafiti wa taasisi ya TechSci ilithaminisha soko la kimataifa la ujenzi huu wa kuwa limefikia bilioni 13 na kutabiri kukua katika kiwango cha uchumi wa kila mwaka (CAGR) cha zaidi ya 11%, ambayo inakaribia dola bilioni 25 ifikapo 2024.
SAFBUILD inaungana bidhaa nyingine za ujenzi za ALAF ambazo ni pamoja ufungaji bora wa paa, ukuta na vifaa vya mwanga, kutenga ukuta kwa vizuizi vya SAFTHERM, karatasi za kupitisha umeme za CLEARDEK polycarbonate, vifuniko vya ukuta na vifaa vya kupamba paa, mfumo wa utoaji maji ya mvua na vifaa vya FIXTITE.
SAFBUILD inatoa huduma bora kwa vitendo inayokwenda sambamba na thamani na gharama ya mteja. ALAF inaahidi kuendelea kuwasiliana na washauri wa mradi huo ili kupata maelezo yote ya kiufundi yanayohitajika katika muundo na utekelezaji wa hatua zote za mradi na kutoa usimamizi wa uundaji kupitia kwenye mtandao ili kuhakikisha ubora na viwango vinafikiwa.
Hii yote ni kutaka kuondokana na soko la mazoea la kutumia vyuma vizito na kuingia katika mfumo wa kisasa ambao ni mwepesi kwa mteja wa SAFBUILD, watengenezaji na watumiaji wa mwisho kwa uwiano sawa wote watafurahia ubunifu wa kiwango cha juu, unaoongoza kwa ujenzi wa haraka na matengenezo ya bure ambayo yatafaidisha vizazi vijavyo.
Muunganiko wa vyuma unatengenezwa katika uwiano sawa ambao wakati wote ufanya mfumo wa jengo kuwa imara. SAFBUILD inasimamia ubora na kuhakikisha inaondoa hofu ya kutokea kwa majanga alimaliza kusema Sumary.
Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa SUMA JKT CCL, Morgan Nyoni alisema tumefurahishwa na teknolojia hii ya kisasa ambayo itakuwa msaada mkubwa sana kwenye kambi zetu, itawezesha kujenga mabweni kwa haraka na unafuu bila katumia matofali na mbao kwa gharama nafuu, na pia itawezesha kuhamisha mabweni pale inapobidi kufanya hivyo.