Club ya Liverpool sasa ishindwe yenyewe kutwaa taji la Ligi Kuu England msimu huu wa 2019/2020, wakiwa wanaendelea kutoa dozi katika kila mchezo wa EPL unaokuja mbele yao, leo walikuwa nyumbani kwao Anfield kuwakabili West Ham United ambao nao walikuwa wanapambania kuwa timu ya kwanza kuifunga Liverpool msimu huu katika EPL.
Bahati mbaya jitihada za West Ham hazikuzaa matunda na kujikuta wakifungwa kwa magoli 3-2, goli la nne la Liverpool likikataliwa na VAR, magoli ya Liverpool yakifungwa na Wijnaldum dakika ya 9, Mohammed Salah dakika ya 68 na Sadio Mane dakika ya 81 wakati ya West Ham yakifungwa na Issa Diop dakika ya 12 na Pablo Folnals dakika ya 54.
Hadi sasa Liverpool wamebakiwa na michezo 11 kumaliza Ligi Kuu wakiwa wanaongoza Ligi wakiwa na point 79, wakiwa wanasubiria ushindi wa mechi nne tu watangaze Ubingwa wa EPL wakiwa na michezo 7 mkononi, kwani wakishinda game 4 zijazo za EPL watakuwa na point ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ya EPL hata Man City akishinda mechi zote atakuwa na point 90 wakati wao kwa kushinda game 4 tu watakuwa na point 91.
Kwa sasa Liverpool wanachotazamia zaidi ni kupambania rekodi ya kuchukua Ubingwa huo bila kupoteza mchezo kama ilivyokuwa kwa Arsenal walivyowahi kutwaa taji hilo msimu wa 2003/4 bila kupoteza mchezo wowote wa EPL ila Arsenal walikuwa wameshinda michezo 26 na sare 12 ila hadi sasa Liverpool wao wana sare 2 hivyo wanaweza kuipiku rekodi ya Arsenal kama watafanikiwa.
VIDEO: ZAHERA AIPA UBINGWA SIMBA, AELEZA HATMA YA LUC EMAEL NDANI YA YANGA