Club ya CD Leganes ilituma ombi kwa shirikisho la soka nchini Hispania (RFEF) la kuomba kufanya usajili wa mchezaji mmoja nje ya dirisha la usajili kama ilivyokuwa kwa FC Barcelona walioruhusiwa kumsajili Martin Braithwaite kama mbadala wa staa wao Ousmane Dembele aliyeumia na kuwa nje ya uwanja kwa miezi sita.
Hivyo Barcelona kwa mujibu wa sheria za RFEF zinaruhusu timu kusajili mchezaji mpya nje ya dirisha la usajili kama itakuwa ina majeruhi atakayekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitano, sasa kutokana na mchezaji huyo kusajiliwa na Barcelona akitokea Leganes walioomba kupewa nafasi na wao ya kufanya usajili ili wazibe pengo lake.
RFEF wamekataa ombi hilo na kusema kuwa hakuna kifungu cha sheria kinachoruhusu wao kupewa nafasi hiyo ikitokea mchezaji wao mmoja akaamua kuvunja mkataba na kuondoka kama alivyofanya Martin, hivyo sasa Leganes watalazimika kumaliza msimu pasipo kusajili mbadala wa Martin.
VIDEO: “MANARA AWE NA ADABU, MIMI MKUU WA WILAYA AKILETA MDOMO SAA 48 ZINAMUHUSU”-JERRY MURO