Muda mfupi baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ikiongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Dkt Magufuli kupitia kikao cha kawaida cha Kamati hiyo kilichoketi leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, DSM kuazimia kumfukuza uanachama Bernard Membe, Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje amewataka Watu watulie na kuahidi kuongolea kufukuzwa kwake hivi karibuni.
“Watanzania wenzangu nimepata habari ya kufukuzwa kwangu kutoka kwenye Chama changu cha CCM. Simu zinamiminika hadi nashindwa kuzijibu. Tulieni! Nitapata muda wa kuongea na wote muda si mrefu”– MEMBE
Akisoma uamuzi wa Kamati Kuu leo Polepole amesema uamuzi huo umekuja baada ya kuwa taarifa za Membe ndani ya chama zinaonesha mwenendo wake tangu mwaka 2014 amewahi kupata adhabu lakini hajajirekebisha.