Serikali ya Italia baada ya kuonekana kuchukua tahadhari mapema ya kuepukana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona, wameamua kuruhusu michezo mbalimbali nchini Italia kuchezwa bila uwepo wa mashabiki.
Taarifa hii inakuja ikiwa ni siku chache zimepita toka ziripotiwe taarifa za baadhi ya mechi za Ligi Kuu Italia Serie hususani za jiji la Milan kuahirisha kwa kuhofia kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona ambavyo kimsingi vimeshaingia Italia.
Moja kati ya tahadhari za mapema zinazoshauriwa ili kupunguza maambukizi ya virusi hivyo ni kuepusha msongamano au kusanyiko kutokana na ugonjwa huo kuenea kwa njia ya hewa, hivyo serikali nchini Italia imetangaza kuwa kuanzia sasa hakuna tukio la kimichezo litakalochezwa mashabiki wakaruhusiwa kuingia uwanjani hadi April 3.
VIDEO: “KAMA UKITAKA UPEPO PANDA BAJAJ, KAMA UKITAKA SOKA PENDA YANGA”-MBOTO