Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua machimbo ya madini ya Boksiti (Bauxite) yaliyopo kwenye eneo la Magamba wilayani Lushoto mkoani Tanga na kuagiza kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Tanga ambapo alifuatana na Waziri wa Madini Doto Biteko na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula.