“Wakuu salaam!! Kesho Asubuhi ni siku ya HUKUMU ya Kesi ya VIONGOZI wa CHADEMA na MIMI nikiwa mmoja wapo.Chochote kinaweza kutokea !!Nimewiwa kutumia nafasi hii kuwaaga RASMI. Itoshe tu kusema, binafsi nimejiandaa kiroho SAFI KABISA KUKABILIANA na chochote kitakacho kuja“
Hayo ndio maneno yanayopatikana kwenye tweet ya mwisho ya Mbunge wa Kawe Halima Mdee ambayo aliiandika usiku wa kuamkia leo kuelekea kwenye siku ya hukumu ambayo inawakabili Viongozi 8 wa CHADEMA pamoja na wa tisa Vicent Mashinji Katibu Mkuu wa zamani wa CHADEMA ambae kwa sasa amehamia CCM.
LIVE: KUTOKA MAHAKAMANI KISUTU HUKUMU YA VIGOGO WA CHADEMA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA