Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa, virusi vya corona vimeifanya mamlaka hiyo kuanza kuangalia vyanzo vingine vya mapato kutokana na kushuka kwa uingizwaji wa mizigo kutoka China.
Akizungumza mara baada ya kutembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam, Kamishna wa Forodha na Ushuru wa bidhaa kutoka TRA, – Ben Usaje Asubisye amesema kuwa, wafanyabiashara wengi wamesitisha kwenda kuchukua bidhaa China, hivyo wanakosa mapato mengi.
Kutokana na kukosekana kwa mizigo inayopita katika bandari ya Dar es salaam kutoka nje, Asubisye amesema ili kukamilisha bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 wanalazimika kuibua vyanzo vipya vya kodi.