Wanafunzi wapatao 3435 wa Shule za Msingi nne zilizopo katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wamesitishiwa vipindi vya masomo yao kwa muda wa wiki moja kutokana na Shule hizo kufungwa kufuatia kuzingirwa na maji mengi ambayo yametokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kutokea kwa maafa ya mafuriko hivyo kunaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao.
Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani Abdul Maulid wakati akizungumza kuhusiana na maafa ya mafuriko hayo amebainishwa kwamba tayari wameshafanya utaratibu kwa wanafunzi wanaosoma darasa la nne na darasa la saba ambao wanatarajia kufanya mitihani yao ya Taifa mwaka huu kuhamishiwa katika Shule ya Msingi Kiwanga ili kuendelea na ratiba ya masomo yao kama kawaida bila kukosa huku juhudi nyingine zikiendelea kufanyika.
KAKA YAKE MSIGWA AFUNGUKA UHUSIANO WAO “MAGUFULI KWETU NI KAYEMBA”