Baada ya kisa kimoja cha corona kuripotiwa Tanzania huku mgonjwa akitajwa kupita katika uwanja wa ndege wa KIA, Hai, Serikali katika Wilaya hiyo imepiga marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima hasa mikusanyiko ya kisiasa .
Wamiliki wa maduka makubwa (Supermarkets) na Bar pia wametakiwa kuhakikisha wanaweka vifaa maalum vya kusafishia mikono vingenevyo maduka hayo yatafungwa.
Uamuzi huo umetangazwa leo na DC Sabaya Lengai Ole Sabaya alipokuwa akizungumza na Viongozi wa makundi mbalimbali.
DEREVA ALIEMBEBA MGONJWA WA CORONA APATIKANA, ALIPELEKA WENGINE KARATU