Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameendelea kutoa taarifa juu ya hatua walizochukua au kufikia hadi sasa baada ya mgonjwa mmoja wa Corona kupatikana Mkoani Arusha.
“Tunatafuta mtandao mzima ambao mgonjwa(Isabella) alishirikiana nao, tumempata Dereva na sampuli yake imepelekwa Maabara, baada ya kumshusha mgonjwa alienda nyumbani akawa na Mke na Watoto , Watoto wakaenda shuleni, Dereva alipata pia wateja wengine”-Gambo