Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kuzingatia maelekezo ya Rais pamoja na Waziri wa Afya kuhusu kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa Corona imeagiza hatua mbalimbali zichukuliwe na mamlaka zake na wadau wa usafiri nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Aloyce Kamwelwe amesema hii leo wakati Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini Kwake Mtumba jijini Dodoma kuhusiana na ya Corona.