Mchezaji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ivory Coast Kolo Toure ana mpango kuandika historia mpya y kuwa kocha wa kwanza raia wa Afrika kuwahi kufundisha EPL.
Toure alikuwa sehemu ya historia katika kikosi cha kocha Arsene Wenger cha msimu wa 2003/2004 kilichotwaa Ubingwa wa EPL bila kufungwa na kuwa club pekee iliyowahi kufanya hivyo England.
”Kuna makocha wengi wa kiafrika katika Ligi mbalimbali kubwa natak kuiwakilisha Afrika nina ndoto siku moja hata timu ya Afrika ichukue Kombe la Dunia hiki ndio ninachokifanyia kazi”>>> Toure
Kwa sasa Toure ni kocha msaidizi wa kocha Brendan Rodgers katika club ya Leicester City ya England, sasa anaamini ndoto yake yaweza kutimia baada ya kuwa na wakati mzuri chini ya Brendan Rodger.