Ubongo Kids ambao wanaongoza kwa utayarishaji wa vipindi vya watoto vya Ubongo Kids, Akili na Me Series, wameguswa na mlipuko wa virusi vya corona na kuamua kushea taarifa muhimu kwa jamii kwa lengo la kusaidia watu wa rika zote hususani watoto wadogo ili kujikinga wakati huu wakiwa majumbani baada ya shule kufungwa.
Kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya elimu (UNESCO) linafuatilia kwa karibu idadi ya watoto walioathirika na mlipuko wa virusi vya corona kwa kukosa muda wa kusoma na kujifunza kutokana na shule kufungwa sababu ya mlipuko wa corona, UNESCO inaeleza kuwa hadi kufikia March 20 idadi ya watoto wanaokosa elimu kwa sasa inafikia bilioni 1.2 kutoka nchi 102 duniani sababu ya shule kufungwa.
Kutokana na changamoto hiyo Ubongo imetoa ofa kutoa mahudhui ya elimu bure kwa watoto na walezi wakati huu shule zikiwa zimefungwa, huku wakiwa hawaruhusiwa kuwa katika mikusanyiko, Ubongo itatoa mahudhui hayo katika mazingira ya ndani watoto wakiwa majumbani kwao.
Wazazi, walimu, walezi na watoto wanashauriwa kutumia njia za kimtandao (Online), TV na Radio kufuatilia episode zote za Ubongo Show (Akili & Me) kwa ajili ya kuwawezesha watoto kujifunza wakati zitakapokuwa zinarushwa hewani Jumatatu saa 10:00 jioni na Jumamosi saa 12:30 asubuhi kupitia EATV.
Kawaida pia vipindi hivyo vimekuwa vikioneshwa Jumamosi na Jumapili kupitia TBC saa 3:00 asubuhi, Akili & Me na Ubongo Kids vitakuwa vinaruka pia katika radio za Bunda FM kuanzia saa 3:00 asubuhi, Uhai FM, Lake FM, Pangani FM itakuwa Jumamosi kuanzia saa 3:00 asubuhi, Baloha FM saa 4:00 asubuhi, TBC Taifa na Highlands ni Jumamosi pia na marudio Jumapili saa 9:00 alasili TBC Taifa, saa 5:00 Micheweni FM, FADECO FM itakuwa saa 8:00 mchana.