Visiwani Zanzibar zaidi ya wasaidizi wa kisheria 100 wamepewa mafunzo kuhusu sheria zilizopo, kanuni, miongozo na sera ambazo zinahusiana na kazi yao ya kisheria huko Zanzibar.
Wasaidia hao wa msaada wa kisheria yaani paralegal wamepewa mafunzo na mbinu ziakazowawezesha kuendelea kutoa elimu na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi nchi nzima bila malipo yoyote na kuwezesha upatikanaji wa haki hasa kwa wanawake
Akizungumza kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria wenzake baada ya mafunzo hayo yaliyofanyika Pemba mwishoni mwa wiki, Rashid Hassan Mshamata kutoka Wete alisema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia sana na kuwapa mbinu mpya za kutumia wakati wa kutoa msaada wa kisheria pamoja na elimu kwenye jamii.
”Mafunzo tuliyopewa ni muhimu sana kwenye kazi zetu za kila siku za kutoa msaada wa kisheria pamoja na elimu kwenye jamii. Tunawashukuru sana waandaaji na tutafanya kazi kufuatia sheria zetu hapa Zanzibar”>>> Mshamata
Wasaidizi wa kisheria wametakiwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo pamoja na kuongeza ushirikiano wa kufanya kazi na serikali pamoja na taasisi zake, aliongeza Mshamata huku akisema wataendelea kutoa msaada na elimu ya sheria kwenye jamii na kuwawezesha wananchi kupata haki zao kwani ni muhimu katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini
Kwa upande wake, Bi Zaina Omari Othman kutoka Micheweni alisema mafunzo hayo yamekuwa zana muhimu ya uwezeshaji kwao katika kutekeleza majukumu yao juu ya msaada wa kisheria kwa jamii.
“Tunafurahi kujifunza vitu vipya ambavyo vimeongeza thamani katika uelewa wetu juu ya maswala kadhaa ya kisheria ambayo yataleta tija katika jamii tunayoitumikia na kutuwezesha kufanya kutoa msaada wa kisheria kwa watu walio na mahitaji maalumu katika jamii,” alisema
Afisa Programu ya Uwezeshaji kutoka Legal Services Facility (LSF) Victoria Mshana alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea ujuzi wasaidizi wa kisheria pamoja na kujua mabadiliko mapya ya kisheria kwa Zanzibar.
“Kutoa mafunzo kuhusu sheria zilizopo, kanuni, miongozo na sera pamoja na mabadiliko ya sheria kutoka siku hadi siku ni moja ya kazi zetu na nimuhimi katika kuhakikisha tunatoa msaada wa kisheria wenye ubora na tija kwa jamii” >>>Mshana
Shirika lisilo la kiserikali la Legal Services Facility – LSF linawezesha upatikanaji wa haki na huduma za msaada wa kisheria kwa kuwawezesha paralegal zaid ya 3950 walioko kila wilaya Tanzania bara na Zanzibar kutoa elimu na msaada wa kisheria kwa jamii bure bila malipo yeyote.
Kwa wastani kwa mwaka paralegal usaidia takribani Zaidi ya kesi 70,000 ambazo asilimia 60 ya kesi hizi wanazitatua wakati asilimia 22 zinakuwa bado zinaendelea asiliamia 16 zimepelekwa kwa vyombo vya juu kwa utatuzi huku asilimia 2 ya kesi zinazowafikia zikishindwa kupatikana usuluhishi.
Kesi zinazotatuliwa kwa wingi na paralegal ni pamoja na kesi za ardhi, ndoa, matunzo kwa watoto, jinai, na ukatili wa kijinsia