Msimu wa Ligi Kuu nchini Ubelgiji wa 2019/2020 umefutwa rasmi huku Club Brugge ikitangazwa kama Bingwa wa msimu, Brugge wamepewa Ubingwa wakiwa na game moja mkononi kabla ya kuanza kwa game za Play off.
Club Brugge kabla ya Ligi Kuu ya Ubelgiji kusimamishwa kutokana na virusi vya corona, walikuwa wakiongoza Ligi hiyo kwa tofauti ya point 15 dhidi ya KAA Gent waliyokuwa wanawafuatia nafasi ya pili.
Maamuzi hayo yatapitiwa tena kuridhiwa April 15 katika mkutano mkuu lakini yamefanyika kupitia mkutano uliofanyika kwa njia ya video conference na viongozi kuamua kupiga kura, mlipuko wa virusi vya corona ndio vimekuwa tatizo kwa Ligi mbalimbali duniani kusimama.