Rais wa Urusi Vladimir Putin ameamuru Watu wa Nchi hiyo kutokwenda kazini na kusalia majumbani hadi mwishoni mwa mwezi huu April kama sehemu ya juhudi za kuzuia kusambaa kwa virusi hatari vya corona.
Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni, Putin amesema anarefusha muda wa kutofanya kazi kwa muda wa wiki tatu zaidi na wafanyakazi wote wanapaswa kulipwa mishahara ndani ya kipindi hicho.
Putin amesema baadhi ya viwanda vinavyozalisha bidhaa muhimu vitaendelea kufanya kazi na maduka ya vyakula na dawa yanaruhusiwa kufunguliwa.
Putin amesema mkakati wa Urusi wa kudhibiti kusambaa kwa corona umefanikiwa lakini ameonya kuwa idadi ya watu walio na maambukizi ya virusi hivyo itaendelea kuongezeka, hadi kufikia muda huu Urusi ina visa 4149 na vifo vya watu 34.
.
Imeandikwa kutoka Idhaa ya Kiswahili