Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amelazwa hospitalini ili kufanyiwa vipimo vya Virusi vya Corona, siku 10 baada ya kukutwa na virusi vya ugonjwa huo, ofisi yake ya Downing Street imesema.
Alikimbizwa katika hospitali moja ya Mjini London siku ya Jumapili (April 5) akionyesha dalili za virusi hivyo ikiwemo kiwango cha juu cha joto mwilini.
Imedaiwa kuwa hatua hiyo ya tahadhari ilichukuliwa kutokana na ushauri wa daktari wake.
Waziri Mkuu bado ndie msimamizi wa Serikali, lakini waziri wa maswala ya kigeni nchini humo anatarajiwa kuongoza mkutano wa virusi vya corona siku ya Jumatatu.
SITA WAKAMATWA KWA MAUAJI YA MWANAJESHI, ATAJWA MWENYEKITI KWA KIFO KINGINE